Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), tayari limetangaza kuanza kwa mchakato kwa wanahabari kutapa vibali maalumu (accreditations) za kushuhudia na kuripoti habari za Fainali za Kombe za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, Juni, 2018.

Kwa wanahabari wanaotaka vibali hivyo hawana budi kujisajili moja kwa moja TFF na wakapata uthibitisho kutoka Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa shirikisho husika na kwa Tanzania, wathibitishwe na Alfred Lucas.

TFF inatoa wito kwa wana habari wenye lengo la kwenda kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia (FIFA World Cup) kuanza mapema machakato huo kwani tarehe ya mwisho kuthibitishwa ni Januari 31, 2018.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.