Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kozi ya awali ya Ukocha kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari imefungwa leo Jumamosi Januari 6, 2018 kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).

Kozi hiyo ya siku Kumi(10) iliyofanyika katika vituo viwili vya Karume na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilishirikisha washiriki Sitini na Tatu(63).

Akifunga kozi hiyo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kanda ya Kigoma na Tabora Issa Bukuku amewataka washiriki kuwa mfano kwa wengine ili nao waweze kupata hamasa ya kushiriki kwenye kozi hizo zitakazosaidia kuwa na makocha wengi watakaosaidia kuanzia ngazi ya Shule.

“Shule ni sehemu sahihi kuwa chachu ya maendeleo ya Mpira wa Miguu kwasababu nyinyi ndio mnawalisha watoto kitu ambacho kitawajengea msingi bora ambao pia utawajenga wakiamini katika masomo na kucheza.”Alisema Bukuku.

Bukuku amesema Kozi za aina hiyo zitaendelea kutolewa chini ya uongozi wa Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia kwakuwa uongozi uliopo sasa madarakani una nia ya dhati kuleta maendeleo ya Mpira wa Miguu kwa vitendo.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma amewataka Wanawake walioshiriki katika Kozi hiyo ya awali kusaidia maendeleo ya soka la Wanawake.

Amesema nia kubwa ni kuendeleza mpira wa Wanawake na kuhakikisha unachezwa ili kufika mbali na kiu ni kucheza mpaka Kombe la Dunia.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi amewataka washiriki kushirikiana na Shirikisho katika maendeleo ya mchezo wa Mpira wa Miguu.

“Kama kuna msaada wowote mnahitaji milango iko wazi muwasiliane nami nawakaribisha kwenye ofisi yangu wakati wowote kwa nia ya kuujenga Mpira wetu.”Alisema Madadi.

Kozi hiyo ya Siku 10 ilifunguliwa Desemba 28, 2017 na kufungwa leo Januari 6, 2018.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.