Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta ameanza mazoezi na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kukaa nje ya Uwanja kwa miezi miwili kufuatia kuumia goti wakati timu yake ikicheza na Lokeren kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji mwezi Novemba mwaka jana.

Kwenye mchezo huo dhidi ya Lokeren Samatta alilazimika kutolewa na kupumzishwa kwenye dakika ya 40 nafasi yake ikachukuliwa na Nikos Karelis mechi iliyomalizika kwa sare ya 0-0.

Samatta amekosa mechi ya timu ya Taifa ilipocheza dhidi ya Benin iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 iliyochezwa huko Benin Novemba 11 2017.

Kurejea kwa Samatta kwenye kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Serengeti yenye ubora wa hali ya juu itaongeza chachu ya ushindi kwa mechi zijazo za Stars.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.