Safari ya Serengeti Boys - timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17, inaendelea licha ya jana Mei 21, mwaka huu kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya kuwania taji la Afrika hapa Port Gentil nchini Gabon.

 

Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na Niger katika mchezo uliofanyika , hivyo kufanya matokeo ya timu zote mbili kufanana kwa pointi, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15, mwaka huu.

Mchezaji wa timu ya Simba SC, Mohamed Hussein amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.

Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.

Washambuliaji Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.

Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14, watapata zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000 kwa kila mmoja.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko taarifa za kupata ajali kwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting FC iliyotokea leo barabara ya Manyoni mkoani Singida wakati kikosi hicho kikitokea Shinyanga kwenda Pwani.

Taarifa kutoka Singida zinasema gari hilo lilipata ajali baada ya tairi moja la mbele kupasuka hivyo kuyumba na kuacha njia eneo la  Itigi - kilometa 200 kutoka Singida mjini kuelekea Manyoni  ambako iliacha njia kitambo ya mita 400 kutoka barabarani kuu kabla ya kugonga mti.

SHEREHE za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kufanyika Mei 24 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo.