Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi kesho Jumatatu,Machi 13, 2017 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga kozi ya ukocha ngazi ya ‘Intermidiate’ kwa makocha 27 wanaotarajiwa kuhitimu.

Kozi hiyo iliyoendeshwa na Wilfred Kidao- Mkufunzi anayetambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), itafungwa saa 5.00 asubuhi kwenye Viwanja vya Michezo vya Bandari, vilivyoko Tandika jijini Dar es Salaam.

Mbali ya Kidao, wakufunzi wengine walikuwa ni Manyika Peter aliyefundisha programu au mtaala kwa makocha wa makipa; Dk. Nassoro Ally Matunzya aliyewanoa makocha hao kuhusu tiba za wanamichezo/wanasoka na Mkufunzi wa mudamrefu wasoka, HemedMteza.

Wanafunzi wa kozi hiyo wanaotarajiwa kuhitimu kesho Jumatatu ni pamoja Doris Malyaga ambaye ni Mwanamke pekee kati ya wanafunzi 27 walisoma kozi hiyo kwa kipindi cha siku 14 cha mwanzo wa mwaka. Doris ni mwana habari za michezo aliyehudhuria kozi hiyo. Anaandikiagazeti la MwanaSPOTI linalotolewa na Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi (MCL).

Wengine ni nyota wa zamani watimu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ waliopata kuchezea klabu kongwe na kubwa nchini. Wanafunzihao ni Boniface Pawasa, Fred Mbuna, Innocent Haule, Herry Morris, Ivo Mapunda, NizarKhalfan na Mussa Hassan Mgosi.

Wengineni Omar Kapilima, AmosiMgisa, UhuruMwambungu, Yussuf Macho, George Minja, Haruna Adolf, SelemaniOmari, Ally Ruvu, MasoudSelemani, Haji Mustapha, MhashamKhatib, IssaNdunje, SalumKapilima, Said Salum, Julio Elieza, Hassan Mwakami, Rajab Mponda, Ally Mbonde na Evod Mchemba