Abou Coulibaly atachezesha mchezo wa pili wa Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Serengeti Boys ya Tanzania na Angola utakaofanyika Uwanja wa l’Amitie kuanzia saa 11.30 jioni kwa saa za Tanzania.

Coulibaly atasaidiwa na Mamady Tere wa Guinea na Attia Amsaad wa Libya wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Mohamed Maarouf wa Misri huku Kamishna akiwa ni Ismael Locate wa Reunion.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ametoa siri ya uimara wa timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 akisema: “Haya yote kayafanya Dk. Harrison Mwakyembe.”

Akizungumza mjini Libreville, Malinzi amesema: “Ujumbe wa kuitakia kheri Serengeti Boys ulitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umeisukuma timu hiyo kufanya vema.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limewateua Watanzania watatu kuwa maofisa waandamizi wa kusimamia mchezo wa kundi A kati ya  Ghana na Gabon wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 utakaofanyika Uwanja wa Port Gentil utakaofanyika kesho Mei 17, 2017.

Watanzania hao ni Mwesigwa Joas Selestine atakayekuwa Kamisha wa mchezo huo wakati Frank John Komba atakuwa mwamuzi msaidizi na katika kitengo cha kitaalamu cha uchunguzi kwa wachezaji wanaotumia dawa za kusisimua misuli atakuwa Dk. Paul Gasper Marealle.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza Makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL). 

Kadhalika TFF, limetangaza timu saba kwa kila kundi katika michuano hiyo itakayoanza Mei 28, mwaka huu katika vituo vya Lindi, Songwe, Tabora na Kahama mkoani Shinyanga.

Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Kusimamia Ligi (Kamati ya Saa 72), iliketi mwishoni mwa wiki iliyopita na kupitia mchezo mmoja baada ya mwingine na kuibuka na uamuzi ufuatao.

Mechi namba 212 (Yanga 2 Vs Kagera Sugar 1). Kamati imefuta kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa mchezaji Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar baada ya kubaini hakutenda kosa lililosababisha mwamuzi ampe adhabu hiyo. Uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(8) ya Ligi Kuu.