Wakati timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kama Serengeti Boys ikirejea salama jijini Dar es Salaam jana jioni, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, leo Februari 8, 2017 wamehamasika kuchagia timu hiyo.

 

Jana asubuhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai alikuwa mstari wa mbele kutoa hamasa hiyo wakati wa matangazo mbalimbali mara baada ya kipindi cha maswali na majibu katika kikao cha bunge.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Wilaya Chunya mkoani Mbeya na Halmashauri ya Mji huo kujenga uwanja bora wa mpira kwa miguu kwa wakazi wa wilaya hiyo.

 

Pongezi za TFF, zimetolewa jana Februari 9, 2017 na Rais wa TFF, Jamal Malinzi alipokutana na uongozi wa wilaya hiyo, aliokutana nao kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambako wote walialikwa na Bunge kwa mambo mbalimbali ya maendeleo.

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo imeondoka kuelekea bungeni Dodoma kwa mwaliko maalumu wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)  inachukua nafasi hii kuishukuru ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuialika timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Boys.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa furaha maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Utendaji ya CAF ya kuipa Tanzania nafasi ya kucheza fainali za Afrika za vijana chini ya umri wa miaka 17 (Afcon U17). Mashindano haya yatanyika nchini Gabon kuanzia tarehe 21 Mei, 2017 hadi 04 Juni, 2017.

 

Timu nane zitashiriki fainali hizi na zimegawanywa makundi mawili, kundi A ni Gabon, Ghana, Guinea, Cameroon na kundi B ni Mali, Niger, Angola na Tanzania. Washindi wawili wa kila kundi wataliwakilisha bara la Afrika katika fainali za dunia huko India mwezi Novemba mwaka huu.


Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72), imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000 (laki tano).

 

Katika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupiga maamuzi ya mwamuzi na kutoa lugha chafu.