Mchezo mmoja wa Azam Sports Federation Cup kati ya Mshikamano na African Lyon – zote za Dar es Salaam unatarajiwa kufanyika kesho Jumatano Februari mosi, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kwamba inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika programu za maendeleo ya vijana, hususani nia yake ya dhati kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.

 

Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari ndiye aliyesema hayo mara baada ya kusikia program za TFF kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mchezaji wa Kagera Sugar, David Abdalla Burhan kilichotokea Hospitali ya Bugando usiku wa kumkia leo Januari 30, 2017.

 

Kutokana na kifo hicho, Rais wa TFF ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi mzima wa Klabu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, familia ya marehemu, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa marehemu Burhan.


Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau kesho Jumatatu Januari 30, kwa pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.

 

Uzinduzi wa kampeni hizo unaopewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’ utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam saa 5.00 asubuhi ambako wadau na wafamilia wa mpira wa miguu wanakaribishwa.

 

 

 

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.

 

Madai ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Simba na Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Taifa, Aprili 11, mwaka jana.