Baraza la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho Alhamis tarehe 16 Julai, 2015 litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Pysical test) kwa waamuzi wa watakochezesha michuano ya kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.  

Zoezi hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi yay a CECAFA.  

Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es salaam, kwa kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati. 

Mashindano ya CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka 1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi anashiriki katika kongamano la Fainali za Dunia kwa Wanawake zinazofanyika Vancouver- Canada kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 - 5 Julai mwaka huu.

Katika kongamano hilo Malinzi ameambatana na katibu mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Amina Karuma.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo. 

Stars ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.

Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes). 

Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.