Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya mwisho wa mwezi Machi mwaka huu, huku timu nane zikichuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Machi 26, 2016 utachezwa mchezo mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakua wenyeji wa wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake ya Zimbabwe, inatarajiwa kuwasili kesho Alhamis mchana wakiwa na msafara wa watu 29, wakiwemo wachezaji 20 pamoja na viongozi 9 tayari kwa ajili ya mchezo wa siku ya Ijumaa dhidi ya wenyeji Twiga Stars uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Zimbabwe watafikia hoteli ya DeMag iliyopo Kinondoni, ambapo jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika uwanaja wa Azam Complex utakaotumika kwa mchezo siku ya Ijumaa.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unaotarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa Machi 04, 2016 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipotembelea kambi ya timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.