Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, kesho jumatano linatarajia kuzindua jezi mpya za timu za Taifa Tanzania, zitakazokuwa zikitumika katika michuano mbalimbali, uzinduzi huo utakafanyika katika hoteli ya JB Belmonte (PSPF) iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo, TFF itawatunukia vyeti viongozi mbalimbali waliotoa mchango katika mpira wa miguu, wadhamini, wahamashisashaji pamoja na wachezaji waliochezea Taifa Stars ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu Tanzania kujiunga na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika -CAF leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.

Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi. 

Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.

TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.

 

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Julai 7 mwaka huu litafungua mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 jijini Mwanza kwa mikoa yote ya Tanzania kwa lengo la kung’amua vipaji kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa  ya vijana wenye umri huo.

Mashindano hayo yatakayofanyika kwa kipindi cha wiki moja, yatafanyika katika viwanja vya CCM Kirumba na Alliance vyote vilivyopo jijini Mwanza, na maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa Mwanza.

 

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.

Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya Airways. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.

Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.

Usajili wa dirisho dogo msimu wa 2014/2015 umefungwa jana (Desemba 15 mwaka huu) huku wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi mbalimbali.

Wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.

Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.

Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.