Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Burundi(FFB) Reverien Ndikuriyo kufuatia kifo cha Kocha Jean Karumba Tigana.

Rais Karia amepokea taarifa za kifo cha Kocha Tigana kwa mshtuko mkubwa.

Kwa niaba ya TFF ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa FFB,Familia,ndugu,jamaa na marafiki wa Tigana.

Amesema mchango wa Kocha Tigana bado ulikua ukihitajika sana kwenye mpira wa miguu Burundi na hata nje ya nchi hiyo.

Kocha Tigana Disemba 22-26,2019 alikua Tanzania alipoiongoza Timu ya Taifa ya Burundi ya Soka la Ufukweni kukamata nafasi ya pili kwenye mashindano Copa Dar es salaam.

Mungu ailaze roho ya Jean Karumba Tigana mahala pema peponi,Amina.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.