Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kikao cha nne msimu wa 2017/2018 cha Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kilichofanyika Novemba 2, 2017 jijini Dar es Salaam, kimefanya mbalimbali kama ifuatavyo.

KATIKA LIGI KUU YA VODACOM

Mechi namba 57 (Azam FC 1 v Mbeya City 0).

Kipa wa Mbeya City, Owen Chaima amesimamishwa kucheza kutokana na kumpiga kofi mshambuliaji wa Azam FC. Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa na Kamati kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Shauri dhidi ya kipa huyo limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

LIGI DARAJA LA KWANZA

Mechi Na. 13 Kundi B (Mawenzi Market 0 v JKT Mlale 1).

Kocha Msaidizi wa JKT Mlale, Rashid Mpenda pamoja na Meneja wa timu hiyo Issa Ngwasho wamesimamishwa wakati wakisubiri suala lao la kumvamia mlemavu wakimtuhumu kwa ushirikina litakaposikiliwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Viongozi hao walifanya kitendo hicho wakati wa mechi dhidi ya Mawenzi Market iliyochezwa Oktoba 7, 2017 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Uamuzi wa kuwasimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Usimamizi wa Ligi.

Mashauri dhidi yao yameletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na yatasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi Na. 22 Kundi B (Polisi Dar 1 v Coastal Union 2).

Wachezaji 16 wa Polisi Dar ambao ni Mpokigwa Mwafubela (15), Emmanuel Mwita (6), Mateso Baraka (7), Magige Belence (10), Ally Mustafa (14), Henerico Sylvanus (16), Paul Makula (9), Paschal Theodory (4), Evance Wilfred (11), Kulwa Said Manzi (20), Athumani Said Mrisho (12), Erick Jafred Mongi (2), Damson Mabala (13), Shabani Haibu Juma (17) na Innocent Edward Barisidya (8) wamesimamishwa hadi suala lao la kumpiga Mwamuzi litakaposikilizwa na kamati ya Nidhamu ya TFF. Uamuzi wa kuwasimamisha umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Pia viongozi wa timu hiyo, Kocha Mkuu William John, Kocha Msaidizi Thabit Kapula, Kocha wa Makipa Eliud Mwalugelo, Mtunza Vifaa Iman Naftari, na Meneja wa Timu Godlisten Kavishe wamesimamishwa wakati wakisubiri suala lao la kumpiga Mwamuzi kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Naye Kiongozi wa Polisi Dar, Mathias Mrimi amesimamishwa kusubiri suala lake la kuhamasisha vurugu dhidi ya Mwamuzi kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Uamuzi wa kumsimamisha ni kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mashauri hayo yameletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na yatasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 23 Kundi B (Mawenzi Market 0 v Mufindi United 1). 

Mtunza Vifaa wa Mawenzi Market, Jumanne Mohamed amesimamishwa wakati akisubiri suala lake la kusababisha vurugu za kutaka kumdhuru Mwamuzi kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Mtunza Vifaa huyo amesimamishwa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Shauri dhidi ya Jumanne Mohamed limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi Na. 25 Kundi B (Coastal Union 1 v Mawenzi Market 0).

Wachezaji wa Mawenzi Market, Ayubu Isaya Sijila (1), Abdallah A. Kulandana (5) na nahodha wa timu hiyo Juma Said Sekubo wamesimamishwa hadi suala lao la kumpiga Mwamuzi litakaposilikizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Hatua ya kuwasimamisha wachezaji hao imezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mashauri dhidi yao yameletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na yatasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 17 Kundi C (Dodoma FC 1 v JKT Oljoro 0).

Wachezaji Shaibu Ally (18), na Frank Kijoti (8) wa JKT Oljoro pamoja na Kocha wao Emmanuel Masawe wamesimamishwa kwa kumfukuza na kutaka kumpiga Mwamuzi hadi suala lao litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Mashauri dhidi yao yameletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na yatasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

LIGI DARAJA LA PILI

Mechi namba 4 Kundi B (AFC 1 v Pepsi 1).

Kocha wa AFC, Gerald Totoo amesimamishwa wakati akisubiri suala lake la kutukana waamuzi na baadhi ya viongozi wa mpira kusikilishwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Pili.

Shauri dhidi yake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 8 Kundi B (AFC 1 v Kitayosce 0). Kipa wa AFC, Aladini Hashimu amesimamishwa, na kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kwenda kwenye jukwaa la washabiki wa Kitayosce na kuanza kupigana. Amesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Pili.

Shauri dhidi yake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 11 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 1 v African Sports 1). Mchezaji Christopher Castor (3) wa African Sports amesimamishwa, na kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kuingia uwanjani na kujaribu kufanya fujo huku akito lugha kali za matusi.  Amesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Pili.

Shauri dhidi yake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 9 Kundi D (Area C 1 v JKT Msange 0). Wachezaji wa JKT Msange, Hosea John (9), Rashid Ally (28), Hamis Athuman (22), Casmir Focus (7) pamoja na Mtunza Vifaa wa timu hiyo Erick Paul wamesimamishwa, na kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kujaribu kumpiga Mwamuzi, lakini pia mchezaji Hosea John alifanikiwa kumpiga ngumi ya shingo Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA).

Mashauri dhidi yao yameletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na yatasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 15 Kundi D (Area C 1 v Mashujaa 0). Mchezaji Katregea W. Kalegea wa Mashujaa FC amesimamishwa, na kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani.

Shauri dhidi yake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mechi namba 1 Kundi D (Nyanza FC 2 v Area C 1). Kocha Msaidizi wa Area C, Omarooh Omari amesimamishwa, na kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumpiga kiwiko mchezaji Rajabu Adam wa Nyanza FC alipokuwa akikimbilia mpira uliopita karibu na Kocha huyo.

Shauri dhidi yake limeletwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na litasikilizwa Novemba 7, 2017 saa 10.00 jioni kwenye ofisi za TFF, Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.