Tanzania yaingia nusu fainali CECAFA U-17
Mechi za hatua ya makundi za mashindano ya CECAFA kwa kundi A zimemalizika leo Juni 17, 2026 katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam ambapo timu ya Tanzania (Serengeti Girls) imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Kenya.
Bao la Serengeti Girls lilipatikana dakika ya 38 kupitia kwa Bahati Kizanguzi katika dakika ya 38 na kuifanya kuongoza kundi lake ikiwa na pointi saba.
Katika hatua hiyo ya makundi, Serengeti Girls ilishinda
mechi mbili, na kutoa sare moja.
Tanzania imefunga jumla ya mabao 15 katika mechi zote tatu wakati Kenya imefunga mabao huku pia ikifikisha pointi saba.
Kenya imeshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa kundi A ikifuatiwa na Somalia ambayo ameshinda mechi moja dhidi ya Sudani. Ilishinda mabao 8-2 huku Sudan ikiburuza mkia baada ya kupoteza mechi zote tatu.
Tanzania itacheza na mshindi wa pili wa kundi B katika hatua ya nusu fainali wakati Kenya itakutana na kinara wa kundi B katika nusu fainali itakayochezwa Juni 21 katika Uwanja wa KMC.
Mechi za mwisho za hatua ya makundi kwa kundi B zitachezwa kesho Juni 18, katika Uwanja wa KMC ambapo Djibouti itakutana na Zanzibar saa saba kamili mchana huku Uganda ikiikabili Sudan Kusini saa kumi jioni.


