Patashika ya Ligi kuu ya wanawake ‘Women’s Premier League’ iliyoendelea leo kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kwa kuwakutanisha watani wa Jadi upande wa wanawake, imeshuhudia Simba Queens ikiitandika bila huruma Yanga Princess mabao saba kwa bila.
Mchezo huo ulikuwa kusisimua kwa dakika zote 90 licha ya Simba Queens kutawala mchezo iliwachukua dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenda mapumziko Simba Queens wakiwa mbele kwa mabao matatu
Mabao ya Simba Queens yaliwekwa kimiani na Mwanahamisi Omari aliyefunga mabao matatu Hat-Trick, pamoja na Amina Ally, Amina Ramadhan huku Frora Kayanda akijifunga (Og) upande wa Yanga Princess ambayo imepanda daraja msimu huu.