WAKATI Ligi Kuu Soka ya Wanawake Tanzania Bara (SWPL) iliyoanza hivi karibuni ikipamba moto, ushindani wa ligi hiyo umezidi kushika kasi.

Ligi hiyo ambayo inadhaminiwa na Bia ya Serengeti Lite, msimu huu imeongezeka utamu kuliko ule wa misimu miwili iliyopita kutokana na kuongezeka kwa michezo ya timu pinzani.

Msimu uliopita upinzani ulikuwa mmoja, kati ya Mlandizi Queens na JKT Queens, lakini msimu huu kuongezeka kwa timu ya Yanga Princess kumeongeza ukali ambapo Simba Queens na Yanga Princess kazi ni nzito.

Katibu wa soka la Wanawake Mkoa wa Pwani, Frolence Ambunisye amesema: “Uwepo wa Yanga Princess unafanya kuwe na upinzani mkali zaidi hasa watakaoupata kutoka kwa Simba Queens.”