TIMU ya JKT Queens imeweka rekodi ya aina yake kwenye Ligi ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kushinda mechi zake zote.

Katika michezo 11 ya mzunguko wa kwanza ambayo wamecheza  wamefanikiwa kujikusanyia pointi 33 wakiwa nafasi ya kwanza.

Kocha wa JKT Queens, Ally Ally amesema lengo kubwa ni kuona wanafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu kwa mara nyingine tena.

“Tunakazi ya kutetea ubingwa msimu huu ndio maana tunacheza kwa tahadhari na heshima kwa timu zote tunazokutana nazo uwanjani.

“Uzoefu wa wachezaji wangu pamoja na mbinu kali ninazowapa zinasaidia tupate matokeo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Ally.