Kamati ya Kimataifa ya mashindano ya SportPesa Cup 2019 jana Jumatano Januari 23,2019 imekaa na kupitia malalamiko ya timu ya AFC Leopards ya Kenya dhidi ya Klabu ya Simba kumtumia mchezaji Lamine Moro jezi namba 17.

Kamati imethibitisha Lamine Moro ni mchezaji halali anayestahili kutumika katika mashindano hayo kwakua ametimiza vigezo vya kutumika.

Lamine amepewa leseni ya muda na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yenye namba 002821M94 iliyotolewa Januari 15,2019.

Kanuni za mashindano ya SportPesa Cup 2019 ibara 5.5 inataka mchezaji anayecheza katika mashindano hayo kuwa na leseni iliyotolewa na Shirikisho la nchi husika anakocheza lakini Shirikisho pia linaweza kutoa leseni za muda kwa wachezaji 3 kushiriki katika mashindano hayo.