Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” leo inafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa marudiano kutafuta tiketi ya kucheza Olimpiki 2020,Tokyo dhidi ya RD Congo.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu Bakari Shime “Mchawi Mweusi” amesema wamekuja Congo kupambana na kupata ushindi.

Shine amesema hakuna majeruhi katika kikosi hicho ambacho kiliwasili hapa Kinshasa jana mchana na jioni wakafanya mazoezi Uwanja wa shule ya Waturuki,Gombe,Congo.

Ameongeza kuwa mapungufu katika mchezo wa kwanza ameyafanyia kazi na wamekuja kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mchezo huo.

Naye nahodha Asha Rashid amesema Wachezaji wamekuja kupambana kuhakikisha wanaiondosha RD Congo.

Amesema kucheza ugenini hakuwapi tabu kwasababu mara kadhaa wameweza kuchukua ubingwa ugenini.

Kikosi hicho kimetua na wachezaji 21 wote wakiwa katika hali nzuri na morali kubwa.

Mchezo utachezwa saa 10 na nusu za jioni sawa na saa 12 na nusu kwa saa za Nyumbani Tanzania na utachezwa Stade des Martyrs