TIMU ya taifa ya Tanzania chini miaka 17 ‘Serengeti Boys’, imepoteza mchezo wake wa kwanza wa makundi wa Total Afcon 2019 U17 dhidi ya Nigeria.
Katika mchezo huo Serengeti Boys wamepoteza kwa kufungwa mabao 4-5, licha ya kupambana vya kutosha ndani ya dakika 90 hasa katika kipindi cha pili baada ya kuingia kwa spidi ya hali ya juu.
Mchezo huu ulitawala ufundi wa hali ya juu kwa timu zote mbili.
Magoli ya Nigeria yalifungwa na Olatomi dakika ya 20, Wisdom aliyefunga magoli mawili dakika ya 29 na 72, Akinkunmi dakika ya 37 na Jabar dakika ya 78, huku magoli ya Serengeti Boys yakifungwa na Edmund aliyefunga mawili dakika ya 21 na 58 kwa penati, Kelvin John dakika ya 51 na nahodha wao Moris Abraham dakika ya 55.
Kesho Serengeti Boys wana mtihani wa kuhakikisha wanashinda michezo yao miwili iliyobaki dhidi ya Angola na Uganda ili kufuzu nusu fainali na kukata tiketi ya kucheza Kombe la dunia la vijana U17 nchini Brazil .