Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inatarajia kuanza Kesho Mei 10,2019 Bariadi,Simiyu.

Timu Nane kutoka katika Vituo 4 vya Simiyu,Katavi,Songwe na Dodoma zitashiriki katika fainali hizo.

Timu hizo zimetokana na Makundi 4 yaliyotoa timu 2 kila Kundi kutengeneza timu 8 zinazocheza hatua ya Fainali kutafuta bingwa wa RCL.

Timu zilizofanikiwa kutinga fainali kutoka katika vituo hivyo ni Bariadi United ya Simiyu itakayokua kwenye Kundi A,Mkurugenzi FC ya Katavi itakayokua Kundi B,Top Boys ya Ruvuma Kundi A,Mji Mpwapwa ya Dodoma Kundi B.

Nyingine ni Mbuni FC ya Arusha Kundi B,Isanga Rangers ya Mbeya Kundi A,DTB ya Dar es Salaam Kundi A na Pan Africans ya Dar es Salaam Kundi B

Timu zimeanza kuwasili kwenye Kituo cha Mashindano.

Waamuzi wote tayari wamewasili.