Timu ya Mji Mpwapwa FC ya Dodoma imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi Mkurungenzi FC ya Katavi, katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa inayoendelea Bariadi,Simiyu

Mchezo huo umechezwa saa 2 asubuhi, kutokana na kushindwa kuchezwa jana kwenye Uwanja wa Halmashauri Bariadi

Deus Moses katika dakika ya 16 na 26 aliiandikia Mji Mpwapwa mabao mawili yaliyodumu mpaka mapumziko

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikiweka tahadhari katika lango lake na katika dakika ya 67 Dick Gembe aliipatia bao Mkurugenzi FC kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Mkurungezi FC Daud Seleman kuchezewa vibaya eneo la hatari na mchezaji Dadi Imbele wa Mji Mpwapwa.

Kamishna wa mchezo huo alikua Ibrahim Kidiwa toka Tanga, Muamuzi wa katikati Abel William kutoka Arusha, Muamuzi msaidizi namba moja Felix Sosthenes wa Mbeya, Muamuzi msaidizi namba mbili Mohammed Msengi kutoka Pwani na Muamuzi wa akiba Tatu Malogo kutoka Tanga,

Leo fainali hizo zinaendelea kwa michezo miwili itakayochezwa Uwanja wa Halmashauri, kuanzia saa 8 mchana.