Benchi la Ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” limeongezewa nguvu kuelekea mashindano ya AFCON yatakayoanza Juni 21,2019 nchini Misri.

Walioongezwa kwenye benchi la Ufundi ni Abdelrahman Essa ambae ni Kocha wa viungo na Ali Taha mtaalamu mwenye ubobevu kwenye kutathmini kiwango.

Essa na Taha wote ni raia wa Misri na tayari wamejiunga kwenye Kambi ya Taifa Stars iliyopo nchini Misri.

Makocha hao wote wawili wamewahi kufanya kazi na Kocha Mkuu Emmanuel Amunike.

Tanzania ipo kundi moja na timu za Algeria,Kenya na Senegal.