Viwango vya Ubora vya Soka la Ufukweni vimetoka na Tanzania ipo nafasi ya 63 Duniani.

Viwango hivyo vimezingatia matokeo ya Soka la Ufukweni kuanzia Juni 2015 mpaka Mei 2019.

Tanzania imefanikiwa kujikusanyia jumla ya alama 163 katika wakati huo wote na kuwafanya kukaa nafasi hiyo ya 63 kwa Ubora wa viwango vya Soka la Ufukweni.

Kutoka Afrika Senegal ndio wapo nafasi ya juu zaidi wakiwa katika nafasi ya 15 na alama 954 wakifuatana na Misri nafasi ya 16 alama 949.

Nchi nyingine zilizo juu ya Tanzania kutoka Afrika ni Nigeria (25),Morocco(27),Madagascar(41),Ivory Coast(44) na Libya(58)

Vigezo vilivyotumika ni michezo ya Kirafiki na ile ya Kimashindano.