Kiungo mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa,Taifa stars,Simon Msuva,amesema wanaimani kubwa ya kupata pointi tatu katika mchezo wa mwisho wa AFCON  dhidi ya Algeria,utakaofanyika,Julai 1 katika Uwanja wa Al- Salam,Misri.

Msuva ,alisema kwamba wapo vizuri na wachezaji wote wanauchukulia kwa uzito huo mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria,kwakuwa wanatambua uwezo wa timu wanayocheza nayo.

“Kwa upande wetu tunamshukuru Mwenyezi Mungu,tupo salama na tunazihitaji sana hizo pointi tatu za Algeria,tunajua wazi kuwa tunacheza na timu nzuri,lakini kwetu tunajua na tunatambua umuhimu wa mchezo wetu huo wa Jumatatu na kwa upande  wetu kila mechi tunaichukulia uzito sawa,kwahiyo Watanzania wasiache kutuombea,na sisi tutajitahidi kucheza kadri ya uwezo wetu kupata kushinda mchezo huo,”alisema Msuva.

Msuva katika mashindano ya mwaka huu ya AFCON ,ndio amekuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Tanzania bao, kwa bao ambalo alilifunga katika mchezo dhidi ya Kenya.