Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetaja kiingilio cha mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu CHAN kati ya Tanzania na Kenya utakaochezwa Uwanja wa Taifa Julai 28,2019.
Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakua shilingi 3000 Jukwaa la Mzunguko linalobeba Watazamaji wengi zaidi,VIP B na C Shilingi 5000.
Tayari Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inaendelea na Kambi iliyopo Hoteli ya APC,Mbweni
Baada ya mchezo huo wa Jumapili Taifa Stars na Kenya watarudiana Agosti 4,2019 Nairobi,Kenya