KIKOSI cha timu ya Taifa Tanzania kimeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Boko Veteran, jijini Dar es Salaam.
Leo ni siku ya pili mfululizo kwa kikosi hiki kufanya mazoezi tangu kitangazwe kwaajili ya mchezo wa kufuzu CHAN dhidi ya Kenya utakaopigwa Julai 28 katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika mazoezi hayo yaliyokuwa yanasimamiwa na kaimu kocha mkuu, Ettiene Ndayiragije alikuwa akiwapa mazoesi mepesi ya viungo pamoja na kuchezea mpira.
Baada ya kuwapa mazoezi mepesi aliwagawanya kwa timu mbili na kisha walicheza kwa takribani dakika 30.
Katika mazoezi hayo alikuwa akiangalia umakini wa mabeki wa pembeni kupiga krosi zitakazoingia ndani ya boksi, lakini vile vile mabeki wa kati kukaba kwa umakini.
Wakati huo huo wachezaji wa timu ya Taifa waliopo katika kikosi cha Simba wanatarajia kuwasili nchini mda wowote na kwenda kambini kujiunga na Timu.
Timu zilivyokuwa Metacha Mnata, Idd Mobby, Masoud Abdalla ‘Cabaye’, Frank Domayo,AbdulaazizMakame, Boniphace Maganga, Ayoub Lyanga na Salim Aiyee.
Juma Kaseja,Kelvin Yondani, David Mwantika, Paul Godfrey ‘Boxer’, Feisal Salum, Paul Ngalema, Idd Seleman ‘Nado’ na Salum Abubakari.