Waamuzi wa mchezo wa kutafuta tiketi ya Fainali za CHAN kati ya Tanzania na Kenya utakaochezwa Jumapili Julai 28,2019 Uwanja wa Taifa wanatarajia kuwasili Kesho Ijumaa.

Waamuzi wa mchezo huo wanatoka nchini Burundi, Mwamuzi wa Katikati atakua Thiery Nkurunziza akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Herve Kakunze.

Katika mchezo huo Mwamuzi msaidizi namba 2 atakua Pascal Ndimunzigo na Mwamuzi wa akiba ni Georges Gatogato.

Kamishna wa mchezo Carlos Francisco Come anatokea nchini Msumbiji.

Kiingilio kwenye mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni ni shilingi 3000 mzunguko na 5000 VIP B na C.