Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeanza kutupa karata yake ya kwanza ya kuitafuta tiketi ya kufuzu CHAN wakitoka suluhu 0-0 na Kenya kwenye Uwanja wa Taifa.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Serengeti Lager ilianza mchezo huo kwa nguvu kutafuta goli hata hivyo mabeki wa Kenya walijitahidi kuzuia mashambulizi hayo.
Ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wake Taifa Stars ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo lakini mpaka mwisho hakuna timu iliyofanikiwa kutumbukiza mpira wavuni.
Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars Ndairagije Etienne baada ya mchezo huo amesema bado wanayo nafasi ya kusonga mbele na sasa wanatazama mchezo wa marudiano utakaochezwa Nairobi baada ya wiki moja.
Amesema Kikosi chake kimecheza vizuri katika mchezo na anaamini Taifa Stars itafuzu ikiwa ugenini ambako watacheza bila ya presha baada ya kutoruhusu goli nyumbani.
Mchezo wa marudiano utachezwa Agosti 4,2019 Nairobi,Kenya