Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” kimeondoka kuelekea Port Elizabeth,Afrika Kusini kwa mashindano ya COSAFA yatakayoanza Agosti 1-11,2019.
Tanzanite iliyopo Kundi B kwenye mashindano hayo imeondoka na Wachezaji 20.
Karata ya Kwanza ya Tanzanite itakua dhidi ya Botswana Agosti 2,2019 ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Eswatini.
Watamaliza hatua ya Makundi kwa kucheza dhidi ya Zambia.
Kocha Mkuu wa Tanzanite Bakar Shime amesema wanakwenda kwenye mashindano hayo wakiwa na lengo la kujifunza,kupata uzoefu na kushindana.