Timu ya Taifa ya Wanawake U20 “Tanzanite” imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa Mashindano ya COSAFA uliochezwa Uwanja wa Gelvalande,Port Elizabeth,Afrika Kusini.

Tanzanite waliandika bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Opa Clement kabla ya Botswana kujifunga kupitia kwa Klaotse kunako kipindi cha Pili.

Katika Mchezo huo mchezaji wa Tanzanite Diana Msemwa ameibuka kuwa mchezaji Bora wa mchezo huo.

Kocha Bakari Shime baada ya mchezo amesema katika dakika za mwanzo walikutana na ugumu kutokana na kutozoea hali ya hewa ya baridi iliyopo Port Elizabeth lakini baadaye waliweza kuendana na hali hiyo.

Amesema wanajipanga kwa michezo inayofuata ya Kundi B dhidi ya Eswatini na Zambia.

Katika mchezo mwingine wa Kundi B Zambia imepata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Eswatini.

Zambia na Tanzania wote wana alama 3 wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.