Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” Bakari Shime ametaja Kikosi cha Wachezaji 23 kwa mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Kenya utakaochezwa Agosti 15,2019 Nairobi,Kenya.

Katika Kikosi hicho amewajumuisha Wachezaji 13 Kikosi cha U20 kilichopo Port Elizabeth,Afrika Kusini kwenye mashindano ya Cosafa yanayomalizika Kesho huku Tanzania ikicheza Fainali na Zambia.

Kikosi hicho kitaondoka Jumanne jioni kuelekea Nairobi.

Kikosi kilichoitwa:

Najat Abas(JKT)
Tausi Abdallah (Mlandizi)
Janeth Shija(Simba)
Fatuma Issa(Evergreen)
Enekia Kasonga(Alliance)
Fumukazi Ally(JKT)
Emeliana Mdimu(Makongo)
Protasia Pius(Ruvuma)
Happy Hezron (JKT)
Irene Kisisa(Kigoma)
Janeth Christopher (Mlandizi)
Donisia Minja(JKT)
Stumai Abdallah (JKT)
Diana Lucas(Ruvuma)
Asha Hamza(Kigoma)
Amina Ally(Simba)
Ester Mabanza(Alliance)
Vailet Thadeo(Simba)
Pheromena David(Mlandizi)
Fatuma Mustapha (JKT)
Opa Clement (Simba)
Mwanahamisi Omary (Simba)
Aisha Masaka(Alliance)