Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Starts” imetinga hatua ya makundi ya michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu kucheza kombe la dunia 2022 Qatar baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Burundi.
Dakika 90 za mpambano huo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuongezwa dakika nyingine 30 lakini hakukupatikana mbabe na ndipo Changamoto ya Penalti ilibidi itumike ili kumpata mshindi wa mtanange huo.
Mbwana Samatta alifunga bao la Taifa Stars dakika ya 29 ya mchezo huku kwa upande wa timu ya Burundi goli likipachikwa kimiani na Abdul Fiston dakika ya 45.
Penati za Stars zilifungwa na Erasto Nyoni,Himid Mao na Gadiel Michael huku mikwaju yao ikipigwa na Saido Berahino,Ngando Omar na Bigirimana Gael.
Mchezo wa awali uliochezwa Bujumbura, Burundi ulimalizika kwa suluhu ya sare 1-1.