Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka 4 na Kampuni ya Azam Media kuonesha mechi za timu ya Taifa “Taifa Stars” inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti.

Mkataba huo una thamani ya shilingi milioni 100 kwa mwaka ambao umegawanywa kwa shilingi Milioni 35 kwa mechi.

Mechi zitakazohusika ni zile za Kirafiki za Kimataifa pamoja na zile za mashindano ambazo haki ipo chini ya TFF.

Katika upande mwingine pia TFF na Azam Media wameingia Mkataba wa miaka 4 unaohusiana na Mashindano ya Azam Sports Federation Cup wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema Azam Media amekua mshirika mkubwa wa TFF kwa asilimia 80.

Amesema mpaka kufikia kusaini mikataba hiyo iliyoboreshwa tofauti na ya nyuma mchakato mzima umepita kwenye vikao mbalimbali kama Katiba inavyotaka na ina baraka zote.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Tido Mhando amesema utiaji saini uliofanyika leo ni dhamira nyingine waliyo nayo huku akisema mafanikio ya haraka kwa Timu ya Taifa na Klabu wana mchango mkubwa ambao wanataka kuendelea kuutoa.