Simba SC ilikuwa Uwanja wa Uhuru kuwakaribisha Mtibwa Sugar na huko Mkwakwani Coastal Union waliwakaribisha KMC.
Kwenye Uwanja wa Uhuru Simba imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mabao ya Meddie Kagere na Miraji Athuman wakati lile la Mtibwa likifungwa na Riphat Khamis.
Mchezo mwingine uliochezwa Mkwakwani Tanga,wenyeji Coastal Union wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC mabao yaliyofungwa na Shaban Idd na Ayoub Lyanga
Kesho VPL inaendelea tena kwa Namungo kuwaalika Singida United,JKT Tanzania watawakaribisha Lipuli wakati Biashara Mara watasafiri mpaka Mwanza kuwafuata Mbao FC.