Waamuzi 38 wanashiriki katika Kozi ya MA ya FIFA inayofanyika Dar es Salaam.
Akizungumza na Washiriki wa Kozi hiyo Makamu wa pili wa Rais wa TFF Steven Mnguto amesema Waamuzi ni Wadau muhimu katika maendeleo ya Mpira wa Miguu.
Amesema Kozi kama hizo ni muhimu na kuwataka Waamuzi kuzingatia na kufanyia kazi ili kuondoa malalamiko na kupunguza mapungufu.
Kozi hiyo ipo chini ya mkufunzi wa FIFA mwenye uzoefu na umahiri mkubwa katika fani hiyo Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini.
Henriques anatoa mafunzo kwa nadharia na vitendo.
Mafunzo hayo yanaingia katika siku ya tatu kesho.