Timu ya Taifa “Taifa Stars” itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda Oktoba 14,2019 Kigali,Rwanda.

Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Kigali utakua kwenye tarehe za Kalenda ya FIFA.

Shirikisho la Soka la Rwanda na TFF zimefikia makubaliano yote muhimu ya mchezo huo.

Wakati huo huo Waamuzi kutoka nchini Burundi watachezesha mchezo wa marudiano wa CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa Uwanja wa El Merriekh,Omdurman.

Mwamuzi wa katikati Thiery Nkurunzinza atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Willy Habimana,Mwamuzi msaidizi namba 2 Shabani Niyungeko na Mwamuzi wa akiba Georges Gatogato.