Kikosi cha Timu ya Taifa “Taifa Stars” leo kimeanza rasmi kambi kwenye Hoteli ya Saphire.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti inajiandaa kwa mchezo wa Kirafiki utakaochezwa kwenye tarehe za Kalenda ya FIFA dhidi ya Rwanda Oktoba 14,2019.

Mchezo huo dhidi ya Rwanda utatumika kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano wa CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa Oktoba 18,2019 El Merriekh Omdurman.

Kocha Ndairagije Ettiene ameita wachezaji 28 wengi wakiwa wanaocheza ndani ili kujiandaa vyema kwa mchezo dhidi ya Sudan.

Kikosi kilichotajwa :

Juma Kaseja -KMC
Metacha Mnata -Young Africans
Said Kipao-Kagera
Salum Kimenya-Tz Prisons
Shomari Kapombe-Simba
Gadiel Michael-Simba
Mohamed Hussein-Simba
Kelvin Yondan-Young Africans
Erasto Nyoni-Simba
AbdulAziz Makame-Young Africans
Bakari Nondo-Coastal Union
Jonas Mkude-Simba
Mudathir Yahaya-Azam FC
Idd Suleiman-Azam FC
Salum Abubakar-Azam FC
Frank Domayo-Azam FC
Muzamil Yassin-Simba
Kelvin John-Under 20
Andrew Simchimba-Coastal Union
Shaaban Idd-Azam FC
Ayoub Lyanga-Coastal Union
Miraji Athuman-Simba
Feisal Salum-Young Africans
Ditram Nchimbi -Polisi Tanzania
Simon Msuva-Al Jadid,Morocco
Abdilaiye Yusuph -Solihull,England
Farid Mussa-Tenerife,Hispania
Himid Mao-ENPPI,Misri