Timu ya Taifa “Taifa Stars” inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti imetua Kigali,Rwanda tayari kuikabli Rwanda “Amavubi” kwenye mchezo wa Kirafiki Jumatatu Oktoba 14 Uwanja wa Kigali.
Mchezo huo ambao unachezwa kwenye tarehe za Kalenda ya FIFA unatumika kama sehemu ya maandalizi kwa TaifaStars inayokabiliwa na mchezo wa marudiano CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa El Merriekh,Omdurman Oktoba 18,2019.
Kocha wa Taifa Stars Ndairagije Ettiene amesema mchezo huo una umuhimu mkubwa katika kutazama marekebisho kuelekea mchezo wa Sudan.
Kocha Ndairagije ameita Wachezaji wengi wa ndani lengo kubwa ikiwa kuweka nguvu kwenye mchezo huo ambao Taifa Stars itakua ugenini.
Katika mchezo wa Kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa,Sudan walipata ushindi wa bao 1-0,Stars itakua na kibarua cha kupindua matokeo hayo.