Timu ya Taifa “Taifa Stars” imetoka sare 0-0 na Rwanda katika mchezo wa Kirafiki uliochezwa kwenye tarehe za Kalenda ya FIFA.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Kigali nchini Rwanda Kocha Ndairagije Ettiene ameutumia kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa marudiano CHAN dhidi ya Sudan utakaochezwa Oktoba 18,2019 El Merriekh,Omdurman.

Kipindi cha Kwanza aliwajumuisha Kikosini Wachezaji wanaocheza soka nje ya Tanzania Himid Mao,Simon Msuva,Farid Mussa na Adi Yusuph kabla ya kipindi cha pili kufanya mabadiliko na kuwaingiza Wachezaji wanaocheza soka ndani ya Tanzania.

Kikosi hicho cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kimeondoka Rwanda kuelekea Sudan kwa mchezo huo wa marudiano wa CHAN

Mchezo wa Kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa,Sudan walipata ushindi wa bao 1-0