Kocha Mkuu wa Taifa Stars Ettiene Ndairagije amempa ruhusa Kiungo Jonas Mkude kuondoka kwenye Kambi ya Kikosi hicho kwenda kushughulikia masuala yake ya kifamilia.
Mkude alitoa taarifa kwa Kocha Ndairagije kuomba ruhusa ya kutojiunga Kambini ili kushughulikia masuala ya kifamilia,ruhusa ambayo alipewa kabla ya kuanza kwa Kambi Jumamosi.
Jana Jumatatu Mkude aliripoti Kambini na kumueleza Kocha Ndairagije kuwa bado hajamaliza masuala anayoshughulikia hivyo Kocha amempa ruhusa nyingine ya kumaliza jambo hilo linalomkabili.
Kulingana na muda mfupi uliobaki kuelekea mchezo dhidi ya Equatorial Guinea Kocha Ndairagije hataweza kuongeza mchezaji mwingine.
Taifa Stars inacheza Ijumaa saa 1 usiku Uwanja wa Taifa mchezo wa kwanza hatua ya makundi kufuzu Afcon 2021.