Timu ya Taifa Taifa Stars imetua nchini Tunisia kwa mchezo wa pili wa Kundi J dhidi ya Libya utakaochezwa Jumanne Novemba 19.

Taifa Stars imetua na Kikosi cha Wachezaji 22 tayari kwa mchezo huo utakaochezwa mji wa Monastir kilomita zaidi ya 200 kutoka Tunis.

Baada ya kutua Tunisia Taifa Stars imesogea mpaka kwenye mji wa Sousse ambao upo karibu zaidi na utakapochezwa mchezo huo ikiwa ni Kilomita zipatazo 22.

Kambi ya Kikosi hicho imewekwa kwenye Hoteli ya Movenpick.

Katika mchezo wa kwanza wa Kundi J Taifa Stars ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea mabao ya Simon Msuva na Salum Abubakar.

Mkuu wa Msafara huo ni Suleiman Haji wa Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF