Waamuzi wanne kutoka Tanzania watachezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kwa Wanawake U20 kati ya Ethiopia na Burundi.

Katika mchezo huo utakaochezwa kati ya Disemba 31,2019,Januari 1,2,2020 Mwamuzi wa katikati atakua Florentina Zablon.

Florentina atasaidiwa na Hellen Mduma na Grace Wamala wakati Jonesia Rukyaa atakua Mwamuzi wa akiba.

Mchezo huo namba 20 utachezwa Ethiopia.