Mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Uganda dhidi ya Tanzania Wanawake U20 utachezeshwa na Waamuzi kutoka Burundi.
Mchezo huo utakaochezwa kati ya Disemba 31,2019,Januari 1,2,2020 Uganda Mwamuzi wa katikati Darlene Nduwayo ambaye atasaidiwa na Fides Bangurambona na Alida Iradukunda,Mwamuzi wa akiba Aline Umutoni wakati Kamishna wa mchezo Tesfaneshi Woreta anatokea Ethiopia.
Mchezo wa marudiano wenyewe utachezwa kati Tanzania ya Januari 17,18 na 19,2020 na utachezeshwa na Waamuzi kutoka Kenya.
Mwamuzi wa katikati Agnet Napangor atakayesaidiwa na Mary Njoroge na Carolyne Njoroge,Mwamuzi wa akiba Carolyne Wanjala na Kamishna wa mchezo Tharcile Uwamahoro kutoka Rwanda