Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamtakia kila la heri Nahodha wa timu ya Taifa “Taifa Stars” Mbwana Samatta katika timu yake mpya ya Aston Villa ya Uingereza.

TFF inaamini Samatta anaendelea kufungua milango kwa Wachezaji wa Tanzania katika mpira wa miguu.

Hatua hiyo sio tu itamsaidia binafsi lakini pia itasaidia katika ngazi ya timu ya Taifa pale anaporudi kuitumikia.

Tunamtakia heri katika majukumu yake mapya kwenye Klabu ya Aston Villa na katika jukumu la kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Duniani.

Pia tunaamini kauli mbiu yake ya “Haina Kufeli” ataendelea kuipigania na kufikia lengo.