Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka Angola kuchezesha mchezo wa kufuzu Afcon 2021 kati ya Tunisia na Tanzania utakaochezwa Stade Olympique de Rades,Tunisia Machi 27,2020.
Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Helder Martins Rodrigues De Carvalho akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Jerson Emiliano Dos Santos, Mwamuzi msaidizi namba 2 Ivanildo Meirelles De O Sache Lopes na Mwamuzi wa akiba Joao Amado Muanda Goma.
Kamishna wa mchezo anatokea Misri,Ahmed Mohamed Megahed Osman.