Kim Poulsen: Lengo ni Moja tu Kufuzu AFCON
Timu ya taifa ya Tanzania“Taifa stars iliyopiga kambi yake katika hoteli ya Tiffany jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 7, 2021 imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa tayari kujiandaa na michezo ya kufuzu AFCON dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.
Kocha mkuu wa“Taifa Stars” Kim Poulsen amesema kikosi chake kimeanza mazoezi kikiwa na wachezaji 23 na wengine watajiunga na kikosi hapo baadae , tunao wachezaji chipukizi na wale wazoefu ambao wamekuwa katika kikosi kwa muda mrefu hivyo kikosi kimeenea na tunajiandaa vizuri ili tuweze kupata matokeo katika mechi hizo maana tuna mtazamo mmoja ulio wazi kwa timu nao ni kufuzu AFCON.
kocha huyu amesisitiza kwamba katika mazoezi hayo atajikita zaidi katika mada tatu muhimu; ya kwanza ni lazima ufunge magoli ili kushinda mechi, ya pili ni kuwa wazuri katika kujilinda maana kama huwezi kujilinda huwezi kufunga na mada ya mwisho ni kuhusu namna ambavyo tunakuwa tunakwenda kutoka kujilinda na kushambulia na kutoka kwenye kushambulia na kujilinda na hivi ndivyo vitu vya kuzingatia kwa timu zinapokuwa zinacheza michezo ya kimataifa. Hivyo kwa mbinu hizo kocha Poulsen anaamini zitazaa matunda licha ya kwamba muda uliobaki ni mchache.
Mchezo wa mwisho kwa Taifa Stars katika michuano hiyo ya kufuzu AFCON ulikua dhidi ya Tunisia ambapo walitoka sare ya goli 1-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Saaam.