Timu za Taifa za Wanawake Kuingia Kambini Rasmi Kujifua Tayari kwa Michuano Mbalimbali ya Kimataifa.
Kocha Mkuu wa Timu za Taifa za Wanawake Bakari Shime hivi karibuni alitaja wachezaji watakaounda vikosi vya timu zinazowakilisha Taifa kwa ajili ya kuanza kambi na mazoezi ya kujiandaa kuelekea mashindano mbali mbali ya kimataifa.
Wachezaji mbalimbali tayari wameisha jumuishwa katika majina yatakayounda timu hizo za taifa za wanawake zikiwemo zile za U17, U20 na Twiga Stars ambao wote watakaa kambi moja kama ilivyoada.
Akizungumza na TFF Habari, kocaha Mkuu wa timu hizo Bakari Shime alisema kuwa huo ni utaratibu waliojiwekea kukutana kila baada ya muda kabla ya mashindano kuanza kwa upande wa Timu za wanawake kwa madhumuni ya kuwaandaa wachezaji kwa kuwaweka pamoja kwa muda mrefu ili waweze kuzoeana zaidi jambo ambalo huwaletea ufanisi wawapo uwanjani.
Kocha huyo aliongeza kuwa utaratibu wa kawaida ambao wao walikuwa wamejiwekea wa kukutana kila baada ya mwezi, tangu mwezi Januari mwaka huu haukuweza kufanikiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza; kwa hivyo hii ni mara ya kwanza kuweka kambi tangu kutengenezwa kwa utaratibu huo mpya.
Kocha Shime alisema kuwa wanatarajia kushiriki michuano ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba, lakini pia kufuzu Kombe La Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka ishirini.
Wakati huohuo kujiandaa kwa kufuzu mashindano ya AFCON kwa Timu ya Taifa ya wakubwa ya Twiga Stars, michuano inayo tarajiwa kuanza mwezi juni mwaka huu.