MAKUNDI FAINALI RCL YAPANGWA, KUANZA KUTIMUA VUMBI KESHO ILULU
Droo ya kupanga makundi ya Fainali Ligi ya mabingwa wa Mikoa(RCL) 2021 imefanyika leo kwenye hoteli ya MM, Lindi.
Timu nane zilizotinga katika fainali hizo zimepangwa katika makundi mawili yenye timu nne kila moja.
Kundi A lina timu za Lindi United ya Lindi, TMA Stars ya Arusha, Copco Veterans ya Mwanza na Temeke Squad ya Dar es salaam.
Kundi B lenyewe lina timu za Nyaishozi FC ya Kagera, Black Stars ya Tabora, Mtwivila FC ya Iringa na Baga Friends ya Pwani.
Fainali hizo zitaanza kutimua vumbi kwa michezo miwili itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Ilulu.
Mchezo wa kwanza Copco Veterans watacheza dhidi ya Temeke Squad saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili kati ya Lindi United na TMA Stars saa 10 jioni.