Samatta Arejea Tena Kukipiga Ulaya

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Ally Samatta amerejea nchini Ubelgiji alipokuwa akicheza katika timu ya GENK kwa ajili ya kujiunga na moja kati ya timu zinazoshiriki ligi kuu baada ya klabu yake ya Fenerbahce iliyo nchini Uturuki kupokea ofa kutoka timu hiyo ya Royal Antwerp ya Ubelgiji, ikimtaka mshambliaji huyo wa kimataifa kutoka Tanzania kujiunga ili kuweza kuitumikia klabu hiyo kwenye msimu huu mpya.

Samatta ambaye hivi sasa ni mali ya Fenerbahce aliwahi kuicheza mpira Ubelgiji alipokuwa anaitumikia timu ya K.R.C.Genk kuanzia mwaka 2016 hadi 2020; ambapo nyota huyo wa Tanzania aliweza kucheza  kwa mafanikio makubwa ambayo ndiyo yalimpelekea mchezaji huyo amabaye pia ni nahodha wa Taifa Stars kuweza kupata ofa ya kwenda kuichezea timu ya Aston Villa ya nchini Uingereza kabla ya kwenda kuitumikia Fenerbahce.

Nahodha huyo anayeichezea pia timu ya ‘Taifa Stars’ nchini alisajiliwa na Fenerbahce akiwa na matumaini ya kufika mbali kisoka akiwa chini ya timu hiyo; jambo ambalo hakuweza kulifikia kwa kiwango alichokitarajia. Samatta amefanikiwa kuifungia timu yake ya Fenerbahce mabao  6 katika jumla ya mechi 33 alizopata nafasi ya kucheza. Kufuatia na  ofa hiyo ya Royal Antwerp Samatta anarudi kwa mara nyingine nchini Uturuki akiwa bado ni mali yao.

Samatta ni kati ya wachezaji wa kitanzania wanao iwakilisha vyema nchi kutokana na uzoefu mkubwa wa kuchezea timu tofauti tofauti katika mataifa mbalimbali huku akiwavutia  pia wachezaji wengine wanao tamani kuyafikia mafanikio aliyonayo. TFF na Tanzania kwa ujumla wanajivunia kuwa na mazao mengi ya wachezaji mfano wa Samatta.

Baadhi ya wachezaji wengine wanakipiga nje ya Tanzania ni; Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-Congo), Simoni Msuva ( Wydad Casablanca-Morocco), Himid Mao ( El Entag El Harby-Misri), Kelvin Pius John (Genk, Ubelgiji ),  Nevatus Dismas (Maccabi Tel Aviv-Israel), Yohana Mkomola (Vorskla-Ukraine), Nickson Kibabage ( Difaa El Jadida-Morocco ),  Athuman Yusuf (Yeovil Towan- Uingereza), ; na wengine wengi.